Shule hizo ni Nyamuge (Mwanza), Twibhoki (Mara), Kwema Modern na Rocken Hill (Shinyanga), Jkibira, St Achileus Kiwanuka, St Severine na Rweikiza (zote Kagera).
Shule iliyoshika nafasi ya kwanza katika shule 10 bora ni Raskazone ya Tanga huku St Anne Marie ya jijini Dar es Salaam ikishika nafasi ya sita.
Pia, wanafunzi sita kati ya 10 waliofanya vyema kitaifa katika mtihani huo pia wanatokea shule za kanda ya ziwa.
Dk Msonde amewtaja watahiniwa 10 bora kitaifa na shule zao kwenye mabano ni Ndemezo Lubonankebe (Kadama-Geita), Innocent Seleli (Carmel-Morogoro), Given Malyango (Tumaini Junior –Arusha), Diomedes Mbogo (St Achileus Kiwanuka-Kagera), Sweetbert John (Mingas-Shinyanga).
Najma Manji (Nyamuge-Mwanza), Beatrice Jeremiah (Mapinduzi B-Mara), Mohamed Abdirahman Mohamed na Luqman Ally (Raskazone-Tanga) na Francisco Maiga (Kadama-Geita).