Kwenye mahojiano aliyoyafanya na kipindi cha televisheni cha KTN, Nameless ameelezea kuhusu ugonjwa huo wa ‘Subarachnoid haemorrhage‘ ulivyomtesa na jinsi alivyoongeza juhudi za kupambana na ugonjwa huo na kukimbizwa katika hospitali ya Agha Khan University Hospital na kuwekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.
“Nakumbuka kushikilia kichwa changu kwasababu nilihisi kama kuna kitu kinaota ndani ya kichwa, sikutaka kujua kama nakufa ‘
“Mama yangu alipigiwa simu na kuambiwa kuwa nipo katika hali mbaya na ilimchukua saa mbili kufika, hakuamini kwasababu aliongea na mimi siku kama ya jana ” >>>Nameless
Nameless alikaa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi kwa siku 10 na baadae kuhamishiwa katika wodi za wagonjwa wa kawaida na kupewa tarifa kuwa hakuwa na damu ya kutosha kichwani na hivyo kuongezewa wiki 3 zaidi kwaajili ya uangalizi
VIDEO: