Imeingia siku ya pili leo tangu tajiri mashuhuri nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla MoDewji atekwe nyara na watu wasiojulikana.
Mo alitekwa jana alfajiri wakati akielekea katika ukumbi wa mazoezi katika hoteli moja ya kifahari jijini Dar es Salaam.
Kwamujibu wa taarifa ya mwisho ya polisi jana jioni, watu 12 wanashikiliwa na jeshi hilo kutokana na tukio hilo huku uchunguzi ukiendelea.
Mamlaka zinatarajiwa kueleza umma leo Ijumaa wamefikia wapi na uchunguzi wao mpaka sasa.
Bado haijafahamika ni akina nani wamehusika na uhalifu huo licha ya mamlaka kusema kulikuwa na wazungu wawili walioshiriki.
Mo, mwenye miaka 43, anakisiwa na jarida la masuala ya kifedha la Forbes kuwa na utajili wa dola bilioni 1.5 kiasi kinachomfanya kuwa tajirinamba moja Afrika Mashariki na tajiri mwenye umri mdogo zaidi Afrika nzima.
Siku ya pili, Mo Dewji Bado Hajapatikana Jitihada za Kumtafuta Zinaendelea
0
October 12, 2018
Tags