Simba si shwari, Kocha Kufukuzwa Muda Wowote


NA ELBOGAST MYALUKO
Baada ya jana kocha Masoud Djuma kukosekana kwenye mazoezi ya klabu ya Simba, uongozi wa klabu hiyo kupitia kwa kaimu Rais wake Salim Abdallah umethibitisha kuwa kuna hali ya kutoelewana kati ya kocha mkuu Patrick Aussems na msaidizi wake.

 Salim amekiri kuwa baada ya hali hiyo kutokea, uongozi wa Simba umejitahidi kusuluhisha na kuwaweka sawa makocha hao lakini imeshindikana, hivyo ndani ya siku chache zijazo utatangaza maamuzi rasmi ambayo yanaweza kuwa ni kuachana na kocha huyo raia wa Burundi.

''Hakuna maelewano kati ya mwalimu mkuu na msaidizi wake, uongozi tumetimiza wajibu wetu wa kukaa nao na kuwaweka sawa lakini hakuna mwelekeo mzuri hivyo ni vigumu kusema kwasasa lakini kadri muda unavyokwenda tutasema hatma'', ameeleza.

Masoud ambaye alijiunga na Simba mwaka 2017 akitokea Rayon Sports ya Rwanda amekuwa akiachwa kwenye mechi za mikoani lakini Septemba 30, 2018, alionekana kwenye benchi la Simba ilipotoka suluhu na Yanga.

Masoud amekuwa kocha msaidizi wa Simba tangu ikiwa chini ya Joseph Omog na baadae alipokuja Pierre Lechantre kabla ya kufukuzwa na hivi sasa anafanya kazi na Patrick Aussems na hawana maelewano mazuri.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad