Steve Nyerere "Unatumia Zaidi ya Milioni 80 Kwenye Birthday kwa Siku Moja kwani Ungekula na Ndugu Zako Wachache Isingetrend''

Steve Nyerere Awapa Makavu Wanawake wa Bongo Movie "Unatumia Zaidi ya Milioni 80 kwa Siku Moja kwani Ungekula na Ndugu Zako Wachache Isingetrend''
Msanii wa filamu Bongo Steve Nyerere amewageuka wasanii wenzake na kuwasema kuwa wanaishi maisha mabaya ya kutishana na matumizi mabaya ya fedha, ambayo yatakuja kuwagharimu hapo baadaye.


Akizungumza na www.eatv.tv, Steve Nyerere amesema wasanii hususan wa kike wana maisha ya kuigiza ambayo huwagharimu kwa kiasi kikubwa, badala ya kutumia fedha hizo kujijengea maisha yao ya kesho

“Dada zetu wana maisha ya show time ya kutishana, unajua ukiwa na maisha ya kutaka kuwatisha wanawake wenzako maisha yako yatakuwa yanaenda hovyo, utakuja kukumbuka baadaye, tuna maisha yale gari zuri, nyumba ya kupanga kwa mwezi milioni, mara mwaka milioni 12, saloon kwa siku mara nne, umejitayarishia maisha ya uzeeni!? Mtu yuko tayari kufanya birthday milioni 80 ambayo ni kitu cha siku moja tu, ungechukua ile hela ukaa na watu wako familia yako mkala mkanywa kwani isingetrend”, amesema Steve Nyerere.

Steve Nyerere ameendelea kwa kusema kwamba wasanii wengi hawakumbuki kujiandalia maisha yao ya uzeeni, matokeo yake huishia kuwa omba omba pale maisha ya usanii yanapofika kikomo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad