Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera wanatarajia kutoa huduma ya kliniki ya Moyo inayotembea (Cardiac Mobile Clinic) katika Mkoa wa Kagera kuanzia tarehe 5 hadi tarehe 11 Novemba, 2018.
Huduma zitakazotolewa ni pamoja na upimaji wa vihatarishi vya Magonjwa ya Moyo, ushauri wa kiafya kuhusiana na Magonjwa ya Moyo, na kutoa rufaa kwa wananchi watakaokutwa na matatizo ya Moyo yanayohitajika kupewa rufaa kuja kwenye Taasisi hiyo kwa uchunguzi wa tiba zaidi.