Tahadhari: Usipokee Vipeperushi Vinavyogawiwa Kwenye Magari Barabarani..Soma Kisa Hichi


Kuna mtu jana usiku alitoka ofcn kwake saa nne akapita shell kuweka mafuta,akatokea mtu akampa kipeperushi jamaa akapokea na kutupia kwenye gari,lkn muuzaji wa mafuta akamuonya kwamba asipende kupokea vipeperushi ni hatari kwa usalama wake.

Kweli baada ya kutoka tu shell akaanza kushindwa kuona,macho yakiwa mazito sana,kidogo agonge,alichokumbuka ni kugeuza kurejea shell na alipofika tu akafungua mlango na kutoka akiwa hoi tayari,na yule muuzaji akawa amepiga simu polisi wa doria ndo kufika na kumsaidia.

Leo nimepokea ushuhuda wa mhusika umenitisha sana.

Kuna mtindo wa wizi umebuniwa,either shell au nje ya hapo,kuna watu wanagawa vipeperushi kwa madereva,inaonekana vina madawa,ukikiweka kwenye gari unalewa na kusinzia in a matter of minutes.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad