Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inamsaka Mkurugenzi Mkuu wa PRIDE, Rashid Malima (65) kwa ubadhilifu wa Sh. bilioni 1.8 za taasisi hiyo.
Aidha, Takukuru inamsaka Mhasibu wa Chuo kikuu kishiriki cha Elimu (Duce) cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kosa la kukimbia na ada za wanafunzi.
Pia takukuru imeanzisha operesheni ya kuwasaka wafanyabishara wanaouza bidhaa katika soko kuu la Kariakoo na kufanya udanganyifu wa risiti za EFD ili kuwachukulia hatua za kisheria.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali, John Mbung'o, amebainisha hayo wakati akungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.