Thierry Henry aibomoa Arsenal

Thierry Henry aibomoa Arsenal
Nyota wa zamani wa klabu ya Arsenal Thierry Henry, ametangazwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Monaco ya Ufaransa na anatarajia kuambatana na kocha wa timu za vijana za Arsenal Patrick Kwame Ampadu.



Henry ambaye kwasasa alikuwa akihudumu kama kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Ubelgiji, ataanza kazi rasmi kama kocha wa Monaco siku ya Jumatatu Oktoba 15, 2018. Hii ni baada ya timu hiyo kumfuta kazi aliyekuwa kocha wake Leonardo Jardim kutokana na matokeo mabovu.

Thierry Henry, mwenye umri wa miaka 41, mbali na kuibomoa Arsenal kwa kuichukulia kocha wake wa timu za vijana Patrick Kwame Ampadu, pia atasaidiwa na kocha wa kikosi cha vijana chini ya miaka 23 cha klabu ya Benfica, Joao Carlos Valado Tralhao.

Henry ni miongoni mwa washambuliaji wa zamani walioacha kumbukumbu katika timu ya Monacho ambako alianzia maisha yake ya soka la ushindani kati ya mwaka 1993 na 1999 akicheza michezo 141 na kufunga mabao 28.

Akiwa mchezaji Henry ameshinda taji la Ligue 1 mwaka 1997 akiwa na AS Monaco, Kombe la dunia 1998 akiwa na Ufaransa, ubingwa wa Euro 2000, EPL mara mbili, 2002, 2004 akiwa na Arsenal, Ligi ya Mabingwa Ulaya 2009 na La Liga mara mbili 2009, 2010 akiwa na Barcelona.

Katika maisha yake ya ukocha akianza na timu ya vijana ya Arsenal, Henry hajafanikiwa kushinda taji lakini anajivunia zaidi kushika nafasi ya tatu kwenye Kombe la dunia 2018 nchini Urusi akiwa kocha msaidizi wa Ubelgiji chini ya kocha mkuu Roberto Martinez.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad