WATALAMU wanalieleza tunda la tikiti maji kwamba, mbali na kuwa chanzo kikuu cha Vitamini A, B6, C na madini ya Potassium, Magnesium na virutubisho vingine vingi, pia, nitunda ambalo lina virutubisho vingine vyenye uwezo wa kuamsha hisia za kimwili na kuondoa matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume.
Matumizi ya tikiti maji, katika namna tofauti. PICHA: MTANDAO.
Wanasayansi wanasema kuwa, tikitimaji lina virutubisho vinavyoweza kuleta mhemuko wa kimwili, mithili ya mtu aliyemeza kidonge cha kuongeza nguvu za kiume.
Tunda hilo linaweza kulainisha vizuri mishipa ya damu na kusimamia mzunguko wa damu mwilini, ili uwe mwepesi na kutokuwa na athari mbaya.
Pia, tikiti maji na vyakula vyenye madini mengi aina ya ‘potassium’ huimarisha misuli mwilini na inawafaa zaidi wana michezo.
Ulaji wa kipande kimoja cha tikiti maji kila baada ya kufanya mazoezi mazito, inaondoa tatizo la kukaza misuli ya miguu.
Tikiti maji tena lina kiwango kidogo sana cha kalori huku, ikiwa na kiasi kikubwa cha maji.
Kirutubisho chake aina ya ‘arginine’, huchochea kwa kiasi kikubwa uimarishaji kinga ya mwili.
Tunda hilo hilo la tikiti zinasaidia kuondoa sumu mwilini inayochangia kumpa mtu uchovu na inapozidi, inasababisha magonjwa ya ini na figo.
Kiafya, inapendekezwa kuliwa na wagonjwa wa presha, kwani ina uwezo wa kushusha shinikizo la juu la damu na wakati huohuo, inaongeza nuru ya macho.
Matikiti yana mchango mkubwa ya kuongeza kinga kubwa dhidi ya magonjwa nyemelezi ya kiwamo yenye hatari kama vile kansa ya matiti, kibofu cha mkojo, mapafu na kansa ya tumbo.