Undani Mtanzania Aliyeua mke Kwa Wivu Uingereza, Afungwa


MAHAKAMA jijini London Uingereza imemuelezea Mtanzania Kema Salum (39) aliyehukumiwa kifungo cha miaka 23 jela kwa kupatikana na hatia ya kumuua mkewe Leyla Mtumwa (35), kuwa ni mtu mwenye historia ya ukatili na alitekeleza azma yake kwa kumchoma mkewe kwa kisu mara 49.

Mahakama hiyo imeamuru pia Salum akishamaliza kifungo atawekewa muhuri unaoonesha ni muuaji kwenye nyaraka zake zote kama vitambulisho. Uamuzi huo ulitolewa juzi na Jaji Richard Marks wa Mahakama Kuu ya Makosa ya Jinai ya Old Bailey, jijini London na kusema ushahidi uliotolewa mahakamani hapo umemtia hatiani mtuhumiwa huyo kwani umedhihirisha Salum ni katili na historia imemhukumu.

Jaji Marks alisema Salum alitekeleza kosa hilo Machi 20 mwaka huu, mbele ya mtoto wa kiume wa Leyla mwenye miaka 12, ambapo alimchoma kwa kisu mara 49 kwenye sehemu mbalimbali za mwili wa mkewe.

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa wakati mtuhumiwa akitekeleza mauaji hayo, mtoto huyo alipiga kelele akimtaka amuache kumkatili mama yake na ndipo alipopiga simu polisi kutoa taarifa za tukio hilo.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Marks alisema Salum ana hitoria ya ukatili ambapo mahakama iliambiwa kuwa alikuwa akimtesa aliyewahi kuwa mkewe ambaye sasa anaishi Dubai, Falme za Kiarabu (UAE).

Mahakama ilisema Salum alitekeleza unyama huo kwa kile alichodai ni wivu kutokana na mkewe huyo kutoka kwenda matembezi na marafiki zake wa kike. Mahakama iliambiwa kuwa Salum alitekeleza azma yake ya mauaji nyumbani kwao mjini Haringey jijini London ambapo alikwenda jikoni kuchukua kisu na kisha kuanza kumchoma nacho mgongoni, kichwani, shingoni na sehemu nyingine za mwili hadi mauti yalipomkuta.

Hata hivyo baada ya Salum kukamatwa alidai alifanya hivyo ikiwa ni njia ya kujilinda huku akikana kutenda kosa hilo, lakini baadaye alikiri kosa hilo. Baada ya mahakama kuelezwa hayo, Jaji Marks alisema mtuhumiwa ni mkatili na alimsababishia maumivu makali Leyla kabla ya kufa.

Mahakama hiyo ilisema Salum alidhamiria kutenda kosa hilo kwa sababu alimchoma Leyla visu mara 49 . Awali, taarifa za tukio la mauaji wa Leyla zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na baadaye taarifa rasmi zikathibitisha kuwa ni kweli Kema Salum maarufu kwa jina la Belly anadaiwa kumuua mkewe aliyemfuata jijini London miezi sita kabla ya tukio.

Gazeti hili lilibaini kupitia mitandao ya kijamii, kufanya mazungumzo na watu wa karibu na Kema pamoja na aliyewahi kuwa mkewe, Amitin Mbamba ambaye walikuwa wakifanya kazi wote Kampuni ya Simu ya Airtel kuwa Salum wakati anaishi Dar es Salaam alikuwa akimfanyia vitendo vya ukatili Amitin.

“Nilikuwa nafanya nao kazi Airtel (Salum na Amitin), wakiwa ofisini utawaona wanapendana sana lakini baadaye tulipata taarifa za maisha yao, Kema alikuwa mnyanyasaji, mpigaji.

Ilifikia wakati anampiga Amitin huku amemvua nguo na kumfunga kamba. Amitin alikuwa anavumilia kwani inadaiwa mwanaume akishampiga huwa anamuomba msamaha sana mkewe, lakini kitendo hicho hadi majirani walikereka nacho na kumsihi Amitin aondoke kwa mumewe Magomeni arudi kwao. Mkewe huyo alichoka mateso akaamua kuacha kazi Airtel bila mumewe kufahamu, akachukua mafao yake akakimbilia Dubai kwa wazazi wake.

Kema alimsihi arudi lakini Amitin aligoma. Hata hivyo wakati kesi hii inaendelea Uingereza, maofisa kule walimtafuta Amitin wakamhoji na naamini imesaidia kwani Kema akiwa mahabusu alijifanya kurukwa na akili lakini alipoambiwa habari za Amitin alishituka na kukiri ameua,” alisema mtoa taarifa.

Tabia za ukatili na hasira za Salum pia zilithibitishwa na baba yake mzazi Kasambula Kema ambaye ni mwanamuziki na anaishi nchini Kenya, aliyesema mwanawe huyo wakati wote alikuwa mtu mgomvi.

Baba huyo akikaririwa akisema, “mwanangu mara zote alikuwa mgomvi, nilikuwa nikimuonya kuhusu tabia yake ya hasira na ni wiki iliyopita tu (wiki moja kabla ya tukio) nilizungumza naye kwa njia ya simu na nilitumia wakati huo kumkumbusha kuwa yuko nchi ya kigeni ambayo haiwezi kuvumilia ugomvi au kupigana”.

Taarifa zaidi zilisema Leyla alisoma Shule ya Msingi Arusha na siku moja kabla ya tukio hilo, alitoka usiku na marafiki zake wa kike na kisha kurejea asubuhi na ndipo alikuta mumewe huyo amekasirika kwa kitendo cha yeye kutoka na kumuacha nyumbani mwenyewe.

Ilidaiwa kuwa wakati Leyla anarudi, alikuwa amesindikizwa na rafiki yake ambaye hata hivyo aliamua kuondoka baada ya kuona ugomvi baina ya wanandoa hao umefikia hatua ya kutishiana.

Kwa upande wa mama mzazi wa Leyla, Hidaya Mtumwa baada ya tukio hilo kutokea alisema anataka mwili wa mwanawe urejeshwe Tanzania kwa maziko, jambo ambalo lilifanyika hivyo na Leyla kuzikwa Arusha. Taarifa zaidi zinasema Salum alisoma nchini Kenya katika Chuo Kikuu cha Nairobi, alishawahi kufunga ndoa mara tatu; moja Zanzibar wakati akifanya kazi Zantel na ya pili Dar es Salaam alipoajiriwa na Airtel. Inadaiwa Salum aliachana na wake hao kutokana n
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad