Mambosasa Asema waliomteka mfanya biashara Mohamed Dewji (Mo) ni wazungu wawili... Ulinzi wawekwa Kila Kona Ili Wasiende Nje ya Nchi

Update: Waliomteka Mo ni Wazungu.... Kamanda Mambosasa Aweka Vizuizi kwa Watekaji Wasitoke Nje ya Nchi
Mfanyabishara maarufu nchini ambaye pia ni muwekezaji wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji (MO) amedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana, saa 11 Alfajiri ya leo.


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Lazaro Mambosasa amesema kwamba wameweka vizuizi kuhakikisha hakuna mtu anayetoka, ili watekaji wasitoke nje ya nchi, na kwamba waliohusika kwenye tukio la kumteka Mo Dewij ni raia wawili wa kigeni (wazungu).

Mambosasa amesema kuwa tayari wameweka vizuizi kuhakikisha hakuna anayetoka, ili watekaji wasitoke nje ya nchi.

Tukio hilo limetokea katika ‘Gym’ ya Colosseum iliyopo Oysterbay jijini Dar es salaam ambapo mfanyabiashara huyo alipokuwa akiingia kufanya mazoezi.

Akizungumza na www.eatv.tv leo asubuhi Oktoba 11, 2018, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, Jumanne Murilo amesema baada ya kupata taarifa za tukio hilo wanafuatilia kujua ukweli wake.

Gari ya mfanyabishara Mo Dewij ikiwa eneo la hoteli ya Collesium ambalo alitumia kufika eneo la Gym.

Kamanda wa Polisi wa kanda maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa ametoa taarifa za awali kwa waliohusika katika utekaji wa mfanyabiashara maarufu Mo Dewji kuwa ni watu wawili ambao ni raia wa kigeni.

Dereva wa Uber (jina linahifadhiwa) amesema aliona  watu wakishuka kwenye gari dogo, hoteli ya Collessium wakiwa wamejifunika usoni, wakapiga risasi moja juu na kumchukua Mfanyabiashara maarufu nchini Mohammed Dewji 'Mo'

Dewji ni mwekezaji wa klabu ya Simba akiwa na hisa 49 na amekuwa akiingia katika chati ya juu ya jarida la Forbes kama miongoni mwa matajiri vijana Afrika.

Kwa upande wake baba mzazi wa Mo Dewij amesema kuwa taarifa za kutekwa mwanae zimempa mshtuko na anatumaini Jeshi la Polisi litafanya kazi yake kwa ufanisi zaidi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad