Upinzani DRC Kumsimamisha Mgombea Mmoja wa Urais

Upinzani DRC Kumsimamisha Mgombea Mmoja wa Urais
Vyama vikuu vya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo vinaazimia kumteua mgombea mmoja wa kiti cha uraisi katika uchaguzi mkuu ujao utakaoandaliwa mwezi Desemba mwaka huu.

Viongozi wa vyama saba vya upinzani wanatarajia kumtangaza mwakilishi wao kufikia Novemba 15 baada ya kuafikiana kuhusu suala hilo katika kikao maalum nchini Afrika Kusini.

Wachambuzi wa siasa za Kongo hata hivyo wanatilia shaka uwezekano wa upinzani kukubaliana kumteua mgombea mmoja wa uraisi atakayewaakilisha katika uchaguzi huo ambao utakuwa wa kwanza wa kupokezana madaraka kwa njia ya demokrasia.

Rais Joseph Kabila anaelekea kuondoka madarakani baada ya kuhudumu kwa mihula miwili.

Chama tawala kimemteua waziri wa zamani wa mambo ya ndani Emmanuel Ramazani Shadary kuwa mgombe wake.

Bwana Kabila alitarajiwa kuachia madaraka karibu miaka miwili iliyopita baada ya muhula wake wa pili kumalizika lakini uchaguzi mkuu ukaahirishwa hatua ambayo ilimfanya kuendelea kuwa madarakani.

Huku hayo yakijiri mamlaka nchini DRC kwa mara ya kwanza zimeruhusu maadamano ya upinzani kufanyika katika mji mkuu wa Kinshasa, leo Ijumaa.

Maandamano hayo ni ya yanashinikiza tume huru ya uchaguzi kutotumia mfumo tata wa kielektroniki wakati wa kupiga kura.


Aliyekuwa mbabe wa kivita na makamu wa raisi wa zamani Jean Pierre Bemba amewasihi wafuasi wake kupinga vikali udanganyifu katika mfumo wa uchaguzi akisema mashini za kielektroniki ambazo tume ya uchaguzi inatumia hazijawahi kutumika popote duniani.

Hata hivyo muungano mkuu wa upinzani onaoongozwa na kiongozi Felix Tshisekedi ambaye atagombea uraisi haushiriki maandamano hayo.

Viongozi wawili wakuu wa upinzani, Jean Pierre Bemba na Moise Katumbi, walifungiwa nje ya kinyang'anyiro cha uchaguzi huo ujao.

Hiki ndicho kikosi 'kilichomuua' Khashoggi
Katika mji wa Lubumbashi ambao ni wa pili kwa ukubwa, kiongozi wa upinzani Moise Katumbi pia alitaka wafuasi wake kuandaman akupinga mashini za kielektroniki za kupiga kura lakini polisi ilitoa onyo kali kwa yeyote atakayeshiriki maandamano hayo.

Mwezi uliyopita Rais Kabila aliahidi Umoja wa Mataifa kuwa taifa hilo litafanya uchaguzi huru na wa haki.

Jean Pierre Bemba kiongozi mkuu wa upinzani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo
Hata hivyo miezi kadhaa kabla atangaze kwamba ataondoka madarakani kulishuhudiwa maandamano ya vurugu huku maafisa wa usalama wakitumia nguvu kupita kiasi kuvunja maandamano hayo.

Wakosoaji wanahofia Kabila anafanya njama ya kuhakikisha mgombea ,Emmanuel Ramazani Shadary, hakabiliwi na upinzani mkali.

Usiku wa Alhamisi maafisa wa usalama waliweka vizuwizi katika barabara kuu ya kuelekea mji mkuu wa Kinshasa na kuanza kufanyia ukaguzi magari

Gavana wa jiji la Kinshasa aliidhinisha rasmi maandamano hayo baada ya kukutana na waandalizi wake.

Seneta wa Upinzani Jacques Djoli, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba waandalizi wa maandamano waliafikiana na polisi kuwa waandamanaji hawatafika wilaya ya Gombe ambao ni makao makuu ya idara nyingi za serikali, balozi za mataifa ya kigeni na biashara za hali ya juu.

Mkuu wa polisi wa Kinshasa Sylvano Kasongo alitoa wito kwa waandamanaji kutozua vurugu akisema "Natutaki kuona umwagikaji wa damu wala vifo katika maandamano haya."

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad