Usain Bolt Ppewa ofa ya mkataba wa kucheza soka

Usain Bolt apewa ofa ya mkataba wa kucheza soka
Aliyekuwa mwanariadha maarufu wa mbio fupi duniani, Usain Bolt amepewa ofa rasmi ya mkataba wa kuichezea klabu ya Central Coast Mariners ya nchini Australia.

Bolt amekuwa akifanya majaribio na klabu hiyo tangu mwezi Agosti mwaka huu, ambapo hivi sasa amepewa ofa rasmi wa kuichezea klabu hiyo kwa mujibu wa wakala wake.

"Kujibu kuhusiana na habari zilizoandikwa, ni kweli Usain amepewa ofa ya mkataba lakini sitoweza kuongeza zaidi ya hapo", amesema wakala wa mchezaji huyo, Ricky Simms.

Usain Bolt alifanikiwa kucheza mechi yake ya kwanza ya kiushindani kwenye klabu yake mapema mwezi huu na kufanikiwa kufunga mabao mawili, jambo ambalo liliwapa matumaini klabu hiyo juu ya kumpa mkataba.

Endapo atasaini mkataba rasmi wa kuitumikia klabu hiyo, ataunganishwa katika kikosi kinachoshiriki ligi kuu nchini Australia (A-League), ligi ambayo imeanza rasmi wiki hii kwa Central Coast Mariners kutoka sare ya bao 1-1 na Brisbane Roar.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad