Uwanja wa Simba SC kukamilika Februari


Uwanja mpya wa Klabu ya Simba unaojengwa katika eneo la Bunju jijini Dar es Salaam, unatarajiwa kumalizika ifikapo Februari mwakani. 

Ujenzi huo unaendelea kama kawaida licha ya kuwapo kwa madai ya kutekwa kwa mwekezaji na mwanachama wa klabu hiyo, Mohammed Dewji 'MO' ambaye ndiye anatoa fedha za kuendesha mradi huo. 

Akizungumza na gazeti hili jana, msimamizi wa ujenzi huo, Danny Matiku, alisema kazi ya ujenzi huo inaendelea kwa kasi kama ilivyopangwa na wanaamini wataikamilisha katika muda uliopangwa. 

Matiku alisema kwa sasa tayari wameshamaliza kazi ya kumwagia kifusi na tayari wameanza kuweka mabomba ambayo yatapitishia maji ili mvua itakaponyesha, yasiweze kutuama kwenye eneo la kuchezea. 

Msimamizi huyo alisema uwanja huo utakuwa ni wa nyasi bandia na kwa sasa pia wameshakamilisha uzio ambao unawatenganisha wachezaji na mashabiki watakaokuja uwanjani hapo. 

"Ujenzi unaendelea kama kawaida kwa sababu hii ni kazi ambayo iko kwenye mkataba, uwanja utakuwa na viwango vinavyotakiwa, tayari tumeshakamilisha kumwaga vifusi na zoezi linalofuata katika eneo hili la kuchezea kutandika nyasi bandia, ukuta wa kubeba uwanja umeshakamilika na huku pembeni tutaweka vyuma," alisema msimamizi huyo. 

Aliongeza kuwa baadaye watawakaribisha maofisa kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) ili kukamilisha vipimo rasmi ambavyo vinaruhusiwa na shirikisho hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad