Uwenda Alikiba Kuachia Wimbo Mwingine kwa Jina la Hela

Alikiba Aja na Kitendawili kingine cha Hela
Inawezekana ukimya wa Alikiba ukawa na kishindo kikubwa hivi karibuni, hii ni baada ya kukaa miezi kadhaa bila kutoa ngoma mpya na kwa upande wa mashabiki wamekuwa wakihoji kuhusiana na  Alikiba kuachia ngoma mpya.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Alikiba amepost picha ikiwa na neno ‘Hela’ na wengi kuhoji kuwa huenda muda wowote Alikiba akadondosha ngoma mpya baada ya “Mvumo wa Radi” aliyoiachia May 11,2018.

Miaka kadhaa nyuma Alikiba aliwahi kuachia ngoma ya “Hela” bila official video, hivyo kwa upande mwingine wa mashabiki wanahisi kuwa ndio video ya ngoma ya ‘Hela’  ndio anaitoa, hiyo ni kwa mujibu wa post yake katika ukurasa wake wa instagram.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad