Khabib Nurmagomedov amefanikiwa kulinda rekodi yake ya kutoshindwa pambano baada ya kumpiga, Conor McGregor katika pambano lililoshuhudiwa leo alfajiri.
Katika pambano hilo la raundi tano, Khabib alisimamisha pambano kwa KO baada ya kumkaba vyema Conor katika raundi ya nne kwenye pambano lao la UFC 229.
Mpiganaji huyo kutoka Urusi anaweka rekodi ya kushinda mapambano yote 27, huku akiweka doa kwa rekodi ya Conor ambaye alikuwa anarejea rasmi kwa mara ya kwanza kwenye mapambano hayo baada ya kujaribu masumbwi na kushindwa dhidi ya Floyd Mayweather.
Hata hivyo, pambano hilo limeweka aibu kwenye mapigano hayo, baada ya Khabib kumshambulia mmoja watu wa timu ya Conor kwa kumrushia kitu ambacho hakikufahamika kwa haraka.
This actually happened. #UFC229 pic.twitter.com/C472LJUBlW— Nathan Waywell (@N_Waywell) October 7, 2018
Hatua hiyo ilisababisha timu ya Conor kumrusha nje ya ulingo Khabib lakini alinusuriwa na walinzi baada ya kuingia mikononi mwa mashabiki wa Conor.
Conor pia alipata majeraha makubwa baada ya baadhi ya mashabiki wa Khabib kuvamia ulingo na kuanza kumshambulia.
Sanchez asimika ‘mkuki’ kumlinda Mourinho, afunguka
Mtangazaji alimtangaza mshindi bila wapiganaji hao kuwa ulingoni, huku muandaaji wa pambano hilo Dana White akikataa kumpa mkanda hadharani Khabib, akidai kuwa hilo lilikuwa pambano lililoisha kwa aibu kubwa.