Vita! Ngumi zatawala uchaguzi Naibu Meya, madiwani wazichapa live



UCHAGUZI wa Naibu Meya wa Manispaa Ilala jijini Dar es Salaam umeingia dosari baada ya kugeuka kuwa uwanja wa masumbwi au uwanja wa vita kutokana na baadhi ya madiwani kuamua kurushiana makonde.

Madiwani wa Manispaa ya Ilala leo walikuwa kwenye uchaguzi wa Naibu Meya baada ya aliyekuwa katika nafasi hiyo Omary Kumbilamoto kujiuzulu na kisha kujiunga CCM.

Kumbilamoto kabla ya kujiunga CCM alikuwa diwani wa CUF Kata ya Vingunguti.Hata hivyo baada ya kujiuzulu na kujiunga CCM Kumbilamoto ameshinda tena udiwani wa kata hiyo na leo amechaguliwa Naibu Meya baada ya kushinda kwa kupata kura 27 huku mpinzani wake kura 25.

Dalili za uchaguzi huo kuingia vurugu zilianza kuonekana mapema tu kutokana na kurushiana maneno kwa pande mbili ambazo zilizokuwa zinashiriki uchaguzi huo.Hata hivyo wakati wa kuhesabu hapo ndipo joto la vurugu liliposhika kasi.

Diwani wa Kata Madizini Senga kupitia Chadema aliyekuwa chumba cha kuhesabu aliamua kutoka chumba cha kuhesabu kura na kisha kupaza sauti akidai  msimamizi wa uchaguzi anaharibu uchaguzi huo.Kauli hiyo ilisababisha Polisi waliokuwa eneo hilo kuingia chumba cha kuhesabia kura kwa ajili ya kulinda usalama.

Hata hivyo wakati wanatoka chumba cha kuhesabia kura ndipo baadhi ya madiwani walianza kurushiana ngumu.Sababu za kurushiana ngumi inatokana na madiwani wa upinzani wakidai mgombea wao ameshinda kiti cha Naibu Meya lakini wanashangaa anatangaza diwani wa CCM ambaye ni Kumbilamoto.Hata hivyo Polisi walifanikiwa kutuliza vurugu hizo na hasa kudhibiti masumbwi yaliyokuwa yanarushwa kutoka kwa diwani wa upinzani kurusha makonde kwa diwani wa CCM.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad