Wachezaji Nane wa Serengeti Boys walamba dili nono Ulaya

Wachezaji Nane wa  Serengeti Boys walamba dili nono Ulaya
Vijana wanane wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' wamepata dili la kufanya majaribio katika vilabu mbalimbali barani Ulaya na nchi za Scandnavia.


Hatua hiyo imekuja baada ya vijana hao kuonesha uwezo mkubwa wa vipaji vyao katika mashindano mabalimbali yakiwemo ya kufuzu michuano ya AFCON kwa vijana kwa kanda ya Afica Mashariki yaliyofanyika mwezi Agosti hapa nchini.

Tayari mchezaji mmoja kati ya hao nane ambaye ni nahodha wa timu hiyo,  Moris Abraham anatarajiwa kuwa wa kwanza kuondoka hapa nchini wiki ijayo kuelekea nchini Denmark ambako atafanya majaribio ya wiki mbili baada ya kukamilisha taratibu za kutumikia nchini humo.

Akizungumza kuhusu ofa hizo na utaratibu wa kuondoka kwa wachezaji hao, Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Oscar Mirambo amesema,

"Kwanini mchakato wa mchezaji mmoja unakamilika na mingine ikiwa haijakamilika ni kwasababu tunajaribu kutengeneza utaratibu kwa maana ya maandalizi ya timu yetu, lakini pia vijana wasikose nafasi ", amesema Kocha huyo.

"Lakini pia kwa vilabu ambavyo vimetoa ofa hizo kwa vijana kwenda kufanya majaribio tunawaambia kimsingi kwamba tunataka tutengeneze utaratibu utakaowezesha vijana hao kwenda kufanya majaribio wakati huohuo wasikosekane kwenye timu za taifa pale tutakapowahitaji kwa maana ya kufanya maandalizi ", ameongeza.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad