Wakimbizi wa Congo waliokuwa wakiishi Angola wakitimuliwa


Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa limesema raia wa Kongo wanaofukuzwa kutoka Angola wanarudi nchini mwao wakiwa katika hali ya kukata tamaa. Wengi wao walikuwa wanafanya kazi kwenye sekta ya madini.

Kwa mujibu wa msemaji wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Babar Baloch, raia wa Kongo wanalazimishwa kuvuka mpaka na kurudi nchini mwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baada ya kufukuzwa kutoka nchi jirani ya Angola. Karibu watu 200,000 wamewasili katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tangu wiki mbili zilizopita.

Idadi hiyo ya watu ni kutokana na uamuzi wa serikali ya Angola ya kuwafukuza wahamiaji wa Kongo, ambao wengi wao walikuwa wakifanya kazi katika sekta isiyo rasmi ya madini katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari huko Geneva, Uswisi, msemaji huyo amesema shirika hilo lina wasiwasi juu ya kuongezeka kwa haraka hali itakayosababisha mgogoro wa kibinadamu katika mkoa wa Kasai, ambako hali tayari ni tete.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad