Watanzania waibuka na medali za dhahabu Japan

Watanzania waibuka na medali za dhahabu Japan
Wanariadha wa Tanzania, Marco Joseph, Fabian Joseph na Amina Mohamed wameibuka na medali za dhahabu katika mashindano ya riadha ya 'Nagai Marathon' yaliyofanyika nchini Japan.



Marco Joseph ameibuka na medali ya dhahabu baada ya kushinda mbio ndefu za umbali wa takribani kilomita 42 huku Fabian Joesph na Amina Mohamed wakishinda katika mbio fupi kwenye mashindano hayo yaliyofanyika Jumapili iliyopita.

Akithibitisha taarifa hiyo, Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Mohamed Kiganja amesema,

"Washiriki zaidi ya 1000 walikuwepo hapo katika mashindano hayo, sisi tuliwakilishwa na washiriki 8 na kati yao, mmoja alipata matatizo ya misuli kwahiyo hakumaliza lakini wengine walifanya vizuri ".

"Kilomita 21 tumepata nafasi ya kwanza, pili na ya tatu, ambapo nafasi ya kwanza ni Amina Mohamed, ya pili ni Rosalia Fabian na ya tatu ni Silvia Masatu. Kwa wanaume, wa kwanza ni Fabian Joseph na nafasi ya pili ameshinda Wilbert Peter", ameongeza.

Kwa upande wa mwanariadha, Marco Joseph amesema kuwa anajisikia furaha kwa kushinda medali hiyo huku aakiamini kuwa atashiriki mashindano ya Olympic yatakayofanyika mwaka 2020 nchini Japan.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad