Watu 1,300 Kuzikwa Katika Kaburi Moja Indonesia

Watu 1,300 Kuzikwa Katika Kaburi Moja Indonesia
Kutoka nchini Indonesia ni kwamba kaburi lenye urefu wa Mita 100 limechimbwa kwa ajili ya kuwazika watu 1,300 waliofariki kwa Tsunami na tetemeko, awali kikosi kilielekezwa kuandaa kaburi la miili 300 lakini maelekezo mapya yametaka kaburi hilo liwe kwaajili ya watu 1,30

Nchi ya Indonesia ilikumbwa na Tsunami na Tetemeko siku ya Ijumaa na mpaka sasa idadi rasmi ya waliofariki ni 832 lakini huenda ikaongezeka kutokana na watu wengi kutoonekana huku juhudi za kufukua vifusi zikiendelea.

Uduni wa vifaa vya uokoaji unaelezwa kuchelewesha kuitoa miili 60 ya watu waliokwama kwenye vifusi vya jengo moja la hoteli iliyoanguka.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad