Takriban watu 50 wamepoteza maisha baada ya trela ya kusafirisha mafuta kugongana na gari ndogo katika barabara kuu magharibi mwa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo.
Ajali hiyo ilitokea karibu na mji wa Kisantu, kati ya mji mkuu Kinshasa na bandari ya Matadi.
Watu 100 walipata majeraha mabaya ya moto kwa mujibu wa Atou Matabuana, gavana wa mkono wa wa Kongo Central.
"Moto ulisambaa kwa haraka na kuteketeza nyumba zilizokuwa karibu,"hii ni kwa mujibu wa redio ya Umoja wa Mataifa ya Okapi.
Barabara katikati mwa nchi zimetelekezwa kwa miaka mingi kutokana na vita.
Mwaka 2012 watu 220 waliuawa wakati trela ya mafuta ilipinduka na kuteketeza vijiji kadhaa.
Daktari kwenye hospitali moja anayewatibu majeruhi alisema hakujakuwa na muda wa kuwapa matibabu waathiriwa.
'Tuanajaribu kuwasaidia lakini kuna wale ambao wanapoteza maisha," Dk Resor alisema.
Mji wa Kisantu uko umbali wa kilomita 120 kusini magharib mwa Kinshasa.