Watu Zaidi ya 18 Wapoteza Maisha Kwenye Ajali ya Treni Taiwan

Watu Zaidi  ya 18 Wapoteza Maisha Kwenye Ajali ya Treni Taiwan
TAKRIBAN watu 18 wamepoteza maisha na 170 wamejeruhiwa baada ya treni ya abiria kutoka katika  njia yake kaskazini-mashariki mwa Taiwan. Mamlaka ya reli imesema inafanyia uchunguzi ajali hiyo iliyotokea katika kaunti ya Yilan siku ya Jumapili.

Watu 366 walikuwa kwenye treni hiyo wakisafiri kati ya Taipei na kaunti ya Taitung wakati mabehewa yote manane yalipotoka nje ya njia. Mamlaka zinasema zimewatoa watu wote kwenye treni hiyo iitwayo Puyuma Express 6432 iliripotiwa kupata ajali hiyo ikikaribia stesheni ya Xinma, karibu na mji wa Su’ao.

Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya reli ya Taiwan, Lu Chieh-shen, ameviambia vyombo vya habari kuwa treni hiyo ilikuwa na miaka sita na ilikuwa na hali nzuri kabla ya ajali kutokea. Haijajulikana mara moja sababu ya treni kutoka nje ya reli yake, lakini mashahidi walisema walisikia kelele kubwa, cheche na moshi. Vikosi vya zima moto vinasaidia majeruhi na wizara ya ulinzi imesema inapeleka wanajeshi 120 kusaidia jitihada za uokoaji.
Shughuli za uokoaji ziliendelea usiku mzima
Mashuhuda walilazimika kuvunja vioo ili kutoka nje ya mabehewa, na baadhi ya waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini.

Mwanahabari kutoka shirika la habari la Ufaransa aliyekuwa kwenye eneo la tukio amesema miili imekuwa ikiondolewa kutoka kwenye mabehewa yaliyoharibika.

Kiongozi wa Taiwan,Tsai Ing-wen, amesema kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa ni tukio baya sana. Taiwan ina mtandao mkubwa sana wa usafirishaji wa treni, na zaidi ya nusu milioni ya abiria husafiri kwa treni kila siku.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad