Watu Zaidi ya 40 Wafariki Katika Ajali ya Basi Iliyotokea Kenya

Watu Zaidi ya 40 Wafariki Katika Ajali ya Basi Iliyotokea Kenya

Watu 42 wamefariki dunia nchini Kenya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupata ajali kwenye barabara kuu ya Nairobi-Kisumu.

Mashuhuda wanasema kuwa ajali hiyo ilitokea leo mwendo wa saa kumi na moja alfajiri.

Vyombo vya Habari nchini Kenya vinaripoti Kuwa ajali hiyo mbaya ilitokea katika eneo la Fort Ternan Kaunti ya Kericho.

Kwa mjibu wa kamanda wa polisi Kaunti ya Kericho, James Mogera, basi hilo lenye uwezo wa kubeba abiria 67, lilitoka barabarani kisha kugonga vizuizi vilivyokuwa kando ya barabara na kubiringia mita 20 kwenye bonde.

Kwa mjibu wa Gazeti la Daily Nation, miongoni waliofariki ni watoto wanane wa chini ya umri wa miaka mitano.

Polisi pia wanahofu kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka kutokana na hali ya baadhi ya majeruhi kuwa mbaya.
Shuhuda mmoja anasema alisikia honi, ikifuatwa na mlio mkubwa wa breki, kisha akawasikia abiria wakipiga kelele.

Baadhi ya majerahu wanatibiwa katika Zahanati ya Fort Ternan, huku wengine wakikimbizwa hadi kwenye Hospitali ya Kaunti mjini Muhoroni kwa matibabu.

Taarifa zaidi zinasema miili ya baadhi ya watu waliofariki ingali imekwama ndani ya mabaki ya basi hilo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad