NAHODHA wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney amesema kuwa tatizo la timu hiyo siyo kocha Jose Mourinho bali wachezaji.
Rooney aliondoka United akaenda Everton na msimu huu anaitumikia DC United ya Ligi K u u ya Marekani, MLS.
Rooney ambaye ana amini k a kuwa ni m c h e z a j i m a k i n i sana, amesema kuwa wachezaji wa timu hiyo wanatakiwa kujitazama upya na kuanza kuipambania timu hiyo na siyo kuacha lawama zote kwa kocha Jose Mourinho.
Rooney amesema kama wachezaji hao wataonyesha kiwango chao basi United inaweza kupata matokeo mazuri uwanjani.
Manchester United wamekuwa na matokeo mabaya kwa siku za hivi karibuni na sasa wapo katika nafasi ya nane w a k i w a na pointi 13 tu wa k iwa w ame s h achez a mi c h e z o nane.
Wikiendi iliyopita timu hiyo ilipata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Newcastle United, ukiwa ni wa kwanza kwao kuanzia Septemba 19.
“Kwa wachezaji wa United na kocha wao huu umekuwa msimu mbaya, najua kuwa wengi wanamyooshea vidole Jose Mourinho, lakini kabla ya hapo wachezaji wanatakiwa kusimama na kuhakikisha wanaipambania timu hiyo.
“Huu siyo mwanzo kwa United kukutana na matatizo haya, hata wakati wa kocha Luis van Gaal tulipita kwenye hali hii hivyo ni jambo la wachezaji kuamka na kuitumikia timu kwa nguvu, waache kulala na kuzembea,” alisema Rooney.