Wazee Simba Waangusha Kisomo Kumuombea Mo Dewji

Wazee Simba Waangusha Kisomo Kumuombea Mo Dewji
ZIKIWA zimepita siku nane tangu mfanyabiashara na mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ kutekwa, jana baraza la wadhamini likiiongozwa na mwenyekiti wake, Mzee Hamisi Kilomoni liliamua kusoma kisomo maalum kwa ajili ya kumuombea. Mo alitekwa asubuhi ya Alhamisi iliyopita katika Hoteli ya Colosseum ambapo alikwenda kwa ajili ya kufanya mazoezi kwenye gym iliyopo hotelini hapo.


Kisomo hicho kilifanyika jana jioni nyumbani kwa mzee Kilomoni Kinondoni Biafra jijini Dar na kuhudhuriwa na baadhi ya wanachama wa timu hiyo ya Simba. Akizungumza na Championi Ijumaa, Mzee Kilomoni alisema lengo kubwa la kisomo hicho ni kumuombea Mo Dewji aweze kunusurika baada ya kutokea kwa tukio la utekwaji.

“Lengo la mimi kufanya kisomo hiki ni kumuombea Mo kwa haya yaliyompata, kama mwenyekiti wa baraza la wazee la Simba, nimeona kwamba kuna sababu ya kufanya hivyo hata kama suala liko katika mikono ya serikali lakini sisi tumeona tumuombee dua kwa Mwenyezi Mungu ili aweze kumnusuru,” alisema Kilomoni. Wiki iliyopita wazee wengine wa klabu hiyo wakiongozwa na mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali, nao walisoma kisomo maalum kwa ajili ya Mo makao makuu ya klabu hiyo Msimbazi, Dar.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad