Wazee wa Jadi Wamfunda Kigwangala, Watoa Onyo kwa Wanaomendea Nafasi Yake

Wazee wa Jadi wWmfunda Kigwangala, Watoa Onyo kwa Wanaomendea Nafasi Yake
Wazee wa kimila na waganga wa jadi wilayani Nzega wameendesha kongamano la kimila kumuombea Mbunge wao ambaye Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamisi Kigwangala huku wakitoa onyo kwa wanasiasa wanaomendea nafasi yake.

Wazee hao kwa pamoja wametoa kauli hiyo hii leo katika dua maalum ya kimila ya kumuombea Mbunge wao iliyofanyika wilayani humo ikiwa ni siku chache baada ya kiongozi huyo kuruhusiwa hospitali kufuatia ajali mbaya ya gari.

Aidha katika kuwashukuru wananchi wa wilaya hiyo, Waziri Kigwangala kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika,

"Hakuna maombi ama dua ambazo sikupokea jimboni siku hizi nne nilizofika kwa mara ya kwanza toka nisalimike kwenye ajali. Ahsanteni sana ndugu zangu kwa upendo na mshkamano mlionionesha".

"Mmenipa nyongeza kubwa sana ya deni kwenu. Nawaahidi kupambania Nzega yetu kwa nguvu zaidi!", ameongeza.

Hatua hiyo imekuja baada ya wananchi wa Nzega kumuomba kiongozi huyo awatembelee kwaajili ya dua pamoja na kuwashukuru kufuatia ajali ya gari ambayo aliipata, Agosti 4 mwaka huu katika kijiji cha Magugu Mkoani Manyara baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kupinduka na kupelekea kifo cha aliyekuwa Afisa Habari wake Hamza Temba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad