Waziri wa ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jaffo amezitaka Halmashauri zipatazo 14 nchini ambazo zimekusanya mapato yake chini ya asilimia 50 kujieleza kwa Waziri huyo kwa kutofikia malengo ya ukusanyaji wa mapato.
Waziri Jaffo amewataka wakuu wa Mikoa kufuatilia baadhi ya mianya ya ufujaji wa fedha ambazo zimekuwa zikipotea katika Halmashauri pamoja na majiji ambayo yameshindwa kufikia malengo katika ukusanyaji wa fedha.
Pia Waziri Jaffo ameelekeza Halmashauri zote nchini zikusanye mapato juu ya asilimia 81 ili kusaidia uboreshaji na utekelezaji wa miundombinu na kuwaagiza wakuu wa Mikoa kusimamia utekelezaji na matumizi ya makusanyo yaliyopatikana.
“Halmashauri zilizoshindwa kufikia mahitaji yao, watendaji wajitathimini huko waliko, imani yangu kila Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya na Halmashauri yake itawajibika mwaka huu wa fedha 2018/2019. Vigezo vyenu vikubwa vitapimwa kwa ukusanyaji wa mapato. ”, amesema Waziri Jaffo.
Katika mkutano huo uliolenga kutoa taarifa za makusanyo ya mapato kwa kila halmashauri na majiji nchini, Waziri Suleiman Jaffo ametaja mikoa iliyofanya vibaya zaidi kwa kukusanya mapato chini ya asilimia 50, ambayo ni Ruvuma, Simiyu na Shinyanga.
Waziri Jafo Azitaka Halmashauri Zilizokusanya Mapato Chini ya Asilimia 50 Kujieleza
0
October 05, 2018
Tags