Waziri Lugola Afunguka Haya Kuhusu Kutekwa kwa Mo Dewji

Waziri Lugola Afunguka Haya Kuhusu Kutekwa kwa Mo Dewji
WAZIRI Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola leo amezungumzia na wanahabari jijini Dar es Salaam na kusema kuwa nchi ipo salama na watanzania waendelee na shughuli zao za kijamii, kiuchumi na kisiasa kwani serikali imejipanga vizuri katika kushughulikia matukio yeyote ya uhalifu yanapojitokeza.



Pia amesema mpaka sasa watu 20 wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya uchunguzi kufuatia tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji jijini Dar es Salaam. Sababu ya kutekwa kwa MO itafahamika pale tu jeshi la polisi litakapompata yeye na kueleza kisa cha kutekwa kwake.



Au itafahamika kirahisi endapo watekaji watakamatwa na kubanwa kuelezea juu tukio hilo.

Watanzania wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii kwa uangalifu na kuacha kusambaza habari zisizo za kweli na taarifa zozote zinazohusu matukio ikiwemo ya upoteaji wa watu zitatolewa na mamlaka za serikali ikiwemo Jeshi la polisi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad