Waziri wa Fedha Afrika Kusini Amejiuzulu Wadhifa Wake kwa Tuhuma za Rushwa Zinazoikabili Familia ya Gupta

Waziri wa Fedha Afrika Kusini Amejiuzulu Wadhifa Wake kwa Tuhuma za Rushwa Zinazoikabili Familia ya Gupta
Waziri wa fedha wa Afrika Kusini Nhlanhla Nene amejiuzulu wadhifa wake baada ya kukubali kuwa aliwahi kukutana na familia ya Gupta ambayo inakabiliwa na mashtaka ya rushwa.

Rais Cyril Ramaphosa amesema amekubali uamuzi wa waziri huyo ili kulinda maslahi ya serikali.

Familia ya Gupta ambayo ni ya wafanyabiashara imekuwa ikituhumiwa kuwa na ukaribu usio wa kawaida na rais wa zamani wa nchi hiyo Jacob Zuma ambapo yadaiwa walishirikiana katika kughushi mikataba ya serikal. Akina Gupta pia yadaiwa walikuwa na ushawishi katika uteuzi wa baraza la mazwaziri.

Ushawishi huo wa kina Gupta ulitafsiriwa kama 'kutekwa nyara' kwa serikali ya Zuma. Ingawa Gupta pamoja na Zuma wamekana madai hayo, lakini yalichangia pakubwa katika msukumo uliopeleka kung'oka madarakani kwa Zuma.

Nafasi ya Nene imechukuliwa na gavana wa zamani wa benki kuu ya nchi hiyo Tito Mboweni.

Hii ni mara ya tano tangu mwka 2014 kwa Afrika Kusini kubadili Waziri wa Fedha.

Wiki iliyopita Nene aliiambia tume ya uchunguzi wa sakata la akina Gupta ijulikanayo kama tume ya Zondo kuwa aliwahi kuhudhuria kikao na wafanyabiasharahao. Awali alikataa katu kukutana na watu hao.

Hakuna mapendekezo ambayo aliyatoa ambayo yako kinyume na sheria wakati alipokutana na wafanyabiashara akiwa anahudumu katika serikali ya Zuma, lakini anakiri kulikuwa na msukumo wa kisiasa ambao umemfanya kuchukua maamuzi ya kujiuzulu.

Nene alifutwa kazi na Zuma mwaka 2015 ikiaminika ni kutokana na ushawishi wa kina Gupta. Mwezi Februari mwaka huu alirudishwa kwenye wadhfa huo na bwana Ramaphosa.


Nene alikutana na wanafamilia wa Gupta katika vikao vya biashara zao nyumbani kwao ndani ya mwaka 2009 na 2014.

Sura ambayo inaonekana ni kuwa waziri wa fedha kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wakubwa inawezekana kuonekana ni kitu cha kawaida lakini akina Gupta wanalalamikiwa kwa kutumia vikao katika makazi yao ya kifahari huko Johannesburg ili kuwashawishi wanasiasa kufanya maamuzi.

Naibu waziri wa fedha wa zamani Mcebisi Jonas aliiambia tume ya Zondo kuwa mwaka 2015 alitunukiwa randi milioni 600 ambayo ni sawa na dola milioni 41 kama angekubali nafasi ya waziri wa fedha katika kikao kilichofanyika katika jumba la kifahari la Johannesburg. Tuhuma hizo pia zimekanushwa na familia hiyo.

Baada ya kufafanua kuhusu vikao vyake,Nene aliomba msamaha kwa umma na kudai kuwa yeye pia ni binadamu hivyo huwa anakosea na hii ikijumuisha kufanya maamuzi mabaya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad