'Whatsapp' Chanzo Cha Kufutwa Matokeo Darasa la 7


Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Taifa (NECTA) Charles Msonde amebainisha sababu ya Halmashauri ya Chemba kufutwa kwa matokeo yake yote  darasa la saba kwa kosa la kuvujisha mitihani hiyo ya kuhitimu elimu ya msingi mtihani uliofanyika Septemba 5 na 6 mwaka huu.


Miongoni mwa mbinu zinazotajwa kutumiwa na halmashauri hiyo ni kuanzisha kwa kundi maalum la Mtandao wa kijamii la Whatsapp lililowaunganisha baadhi ya viongozi wa elimu wa halmashuri hiyo wakiwemo Maafisa Elimu na Waratibu wa Elimu Kata.

Kwa mujibu Charles Msonde Halmashauri hiyo ilikusudia kuongeza ufaulu kwa shule za msingi zilizopo wilayani humo ambapo walishirikiana na wakuu wa shule zilizopo kwenye Halmashauri hiyo.

“Katika kutekeleza azma hiyo siku moja kabla ya mtihani kufanyika mitihani ilifunguliwa na kusambazwa kwenye kundi la whatsapp ili kupandisha ufaulu wa halmashauri, tumegundua viongozi wa elimu wa halmashauri ya Chemba walihusika kwa hali na mali ili kwenye uharifu huo.”

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tamisemi Nixon Mzunda ameagiza kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kwa maafisa elimu na waratibu elimu kata katika Halmashauri na kufikishwa mahakamani kwa kufanya kosa la jinai.

“Ni tukio la kimaadili na tukio lisilovumilika, limetutia aibu na linajenga rasilimali watu wasiokuwa na uadilifu, tumeamua Tamisemi kutengua maafisa elimu wote waliohusika kwenye kusimamia mitihani katika halmashauri ya Chemba na waratibu kata wake, na hatutaishia hapo tumeiviomba vyombo vya dola viendelee kuchukuwa hatua, kwa sababu wanatuingiza gharama bure.”Amesema Nixon Mzunda

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad