Mechi hiyo itakayokuwa maalum kumuaga aliyekuwa mchezaji na nahodha wake, Nadir Haroub 'Cannavaro' inasubiriwa kwa hamu na wadau wa soka visiwani humo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mashindano, Hussein Nyika, amesema kuwa wao tayari wameshajipanga kuelekea mchezo huo.
Nyika amesema kikosi chao kimeshakamilisha mazoezi na sasa wapo tayari kwa mechi hiyo ambayo itaanza majira ya saa 10 kamili.
"Sisi tupo tayari kwa mechi hiyo, kikosi kipo Zanzibar na tunasubiria muda wa mechi ili tuweze kutoa burudani nzuri kwa mashabiki na wanachama wetu kuungana kumuaga Cannavaro''. Alisema.
Yanga inaenda kucheza na Malindi ikiwa haina Kocha wake Mkuu, Mkongomani, Mwinyi Zahera ambaye alisafiri kuelekea Congo kwa majukumu ya kitaifa.
Msaidizi wake Noel Mwandila ndiye atakuwa mkuu wa benchi la ufundi kwa kesho kukipima kikosi kuelekea mechi ijayo ya ligi na Alliance Schools ya Mwanza.