Yanga Waanza Mazungumzo Upya na Ajibu


Uongozi wa Yanga tayari umeanza mazungumzo ya siri na kiungo wao mshambuliaji fundi, Ibrahimu Ajibu kwa ajili ya kumuongezea mkataba mpya wa kuichezea timu hiyo. Hiyo, ikiwa ni siku chache baada ya kuwepo na taarifa za Simba kuanza harakati za kutaka kumrejesha katika timu hiyo aliyoachana nayo kwenye msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara. 

Ajibu ni kati ya wachezaji tegemeo hivi sasa ndani ya Yanga kutokana na kiwango Yanga SC yamwekea Ajibu mkataba mezani kikubwa alichoanza kukionyesha katika msimu huu wa ligi akihusika kwenye mabao nane kati ya 11 waliyofunga akipiga asisti sita huku akifunga mabao mawili pekee. 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano kutoka ndani ya Kamati ya Usajili ya timu hiyo, Yanga wamefikia hatua ya kuanza naye mazungumzo baada ya kubakiza miezi sita katika mkataba wake. 

“Lipo wazi kabisa, Ajibu bado mchango wake unahitajika na kamwe hatutamuachia mchezaji yeyote mwenye umuhimu anayetoa mchango kwa mafanikio ya timu kama alivyo Ajibu. “Tayari kocha mwenyewe ametoa mapendekezo ya baadhi ya wachezaji anaowataka na asiowataka ambao mikataba yao imemalizika na wale waliokuwa nayo kwa ajili ya kuwatoa kwa mkopo. 

“Kocha tayari amependekeza mkataba wa Ajibu uboreshwe kwa maana ya kumuongezea mwingine kwa ajili ya kubaki kuendelea kuichezea Yanga katika misimu mingine ijayo, yaani ni sawa na kusema kuwa tumeshamwekea mezani kazi yake ni kuujaza tu,” alisema mtoa taarifa. 

Alipotafutwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Mkongoman, Mwinyi Zahera kuzungumzia hilo alisema: “Ajibu ni kati ya wachezaji wangu waliopo katika kiwango kizuri tangu kuanza kwa msimu huu. “Hivyo, nimefuatilia mikataba ya wachezaji na kugundua kuwa Ajibu ni muhimu na anatakiwa kubaki. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad