Kaburi lenye miili ya watu 75 limegunduliwa nchini Libya. Miili hiyo inashukiwa kuwa ya wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS. Maafisa nchini Libya wamegundua kaburi lililozikwa watu wengi linaloaminika kuwa na miili 75 ya wapiganaji wa kundi la Dola la Kiislamu karibu na mji wa pwani wa Sirte, ambao hapo zamani ulikuwa ngome kuu ya kundi hilo la itikadi kali katika Afrika Kaskazini.
Msemaji wa jeshi la nchi hiyo katika eneo la Benghazi , Salem el-Ameel , amesema mkaazi mmoja aliripoti kuhusu kaburi hilo kiasi ya mwezi mmoja uliopita katika shamba katika wilaya ya al-Daheir, mashariki mwa Sirte.
Ameongeza kwamba wale waliopatikana katika kaburi hilo wanaonekana kuwa wamevaa nguo za wapiganaji wa IS, lakini uchunguzi wa kitaalamu unahitajika kubaini wao ni nani na wanatoka wapi.
Katika tukio jingine, jeshi hilo linalojitambulisha kuwa jeshi la taifa la Libya limesema limekamata meli mbili za uvuvi za Italia katika pwani ya Libya.
Zaidi ya miili ya watu 74 yakutwa katika kaburi moja nchini Libya
0
October 13, 2018
Tags