AKIWA anaelekea katika kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa jijini London, Zari ‘The Bosslady’, ambaye ni mama watoto wa staa wa muziki wa Bongo, Diamond Platnumz, amepata misukosuko katika uwanja wa ndege wa Heathrow, London, kuhusiana na masuala ya uhamiaji.
Maofisa wa uhamiaji uwanjani hapo walimshikilia kwa saa 16 wakitaka kufahamu kuhusu habari kwamba alitumia pasipoti feki kwenda Uingereza na kwamba umri wake ni miaka 43 na si 38. Hii ni kutokana na habari zilizoenezwa kwenye mitandao ya kijamii.
Hata hivyo, katika kupuuza madai hayo, Zari aliposti ujumbe usemao:
“As for the USA illegal immigrant on social media in the name of being a social media keyboard warrior, I know you’re choking slowly, but then you forgot, It’s me Zari the BossLady.”
“Thank you Lord for my bday. Another homeless wh_re out there posting ma Gov doc. Bi_ch its 1980 whether u like it or not. I did day for my citizenship reasons. Again am glad to give you sleepless night bwahahaha 43 yr old don’t look like me.”
Kutokana na kuchelewa kwake uwanja wa ndege, haifahamiki iwapo aliwahi chereko zilizotangulia siku yake ya kuzaliwa kweye ukumbi wa KingsBull Luxury Lounge, lakini siku iliyofuata ambayo ndiyo ya kuzaliwa kwake, Zari aliungana na mashabiki wake huko Woodgreen ambako aliwashukuru kwa kuhudhuria hafla hiyo. Ujumbe huo aliouandika kwenye mtandao ulisomeka:
“Thank you to all my London fans for celebrating my bday…it’s a beautiful journey with you. 38 has never looked this good #ProudMom.”
Naye Diamond Platnumz, alimtumia Zari ujumbe maalum kuhusiana na siku yake hiyo ya kuzaliwa akimshukuru na kumpongeza kwa kuwa mama watoto wake wawili.
“A very special birthday to the mother of my beloved kids…Thank you for blessing me with 2 amazing & cute kids and thank you for continuing to be a good mother to my children.”
“Trust me, no matter how crazy & a proud man you think I might be, am always grateful and I do respect you for that, that’s why, you’ve never heard or seen me on any interview talking anything about you, not even talking about what happened to us!!…coz the kids you blessed me with, mean a lot to me, and that is what made me love, respect and take you more than a blood sister / Brother for Life! May God bless you with long life, Happiness, and More Winning!”
Zari Azuiliwa Londoni Kisa Kufoji Umri na Pasipoti Feki
0
October 02, 2018
Tags