Zitto Kabwe aungana na Waziri Lugola

Zitto Kabwe aungana na Waziri Lugola
Mbunge wa Kigoma mjini ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola aliyehutubia akiwa wilayani Uvinza mkoani Kigoma ndiye Kangi halisi na si mwingine.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii Zitto amempongeza Waziri Lugola kwa agizo alilolitoa wakati akihutubia wananchi wa Uvinza ambapo aliagiza Jeshi la Polisi kutoa dhamana kwa raia muda wote siku saba za wiki.

Zitto ameandika "Kangi Lugola aliyezungumza akiwa Uvinza Kigoma ndio Kangi wa ukweli. Afisa Polisi aliyejiuzulu kazi kwa kulazimishwa kuachia majambazi aliyewakamata. Mbunge aliyekuwa akitaka reform ya Polisi. Huyu ndiye Kangi halisi. Aendelee kuwa Kangi halisi. Dhamana kwa raia 7/7 days".

Septemba 30, Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola, alitoa agizo kwa Jeshi la Polisi Nchini kuhakikisha dhamana kwa watuhumiwa inatolewa kwa saa 24 katika siku zote 7 za wiki, tofauti na zamani ambapo ilikuwa inatoka mwisho Ijumaa jioni.

Lugola alitoa agizo hilo wakati akiongea na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Basanza wilayani Uvinza, Mkoani Kigoma, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad