Alberto Msando "Nilifeli Darasa la Saba"


From @albertomsando - 08.11.1979 saa 11.45am nimeambiwa nilizaliwa. Leo nimetimiza miaka 39. Nalazimika kujipa muda kidogo kutafakari kuhusu miaka hiyo 39 hapa duniani. Lengo ni kuona kama kuna jambo napaswa au naweza kulifanya tofauti kwa miaka iliyosalia mbeleni ambayo sijui ni mingapi.
Kwa kipindi chote cha miaka 39 nimeishi kwa furaha na huzuni. Vyote nimeweza kuishi navyo mpaka leo. Jambo la msingi kwangu leo hii ni kuangalia pale ambapo nilipaswa kuwa bora zaidi badala ya pale ninapodhani nimefanikiwa. Kuna maeneo mengi ambayo ningeweza kufanya zaidi ya yale niliyofanya. Imani yangu ni kwamba ilipaswa kuwa hivyo ili leo niwe hapa. Chochote kingekuwa tofauti basi leo nisingekuwa hapa. Thats the simplest way of looking at failure. And may be the positive one too.
Nina mfano hai kuhusu hili. Nakumbuka nilifeli (au sikuchaguliwa baada) darasa la saba kwenda Shule ya Serikali. Kwa ‘kufeli’ huko nikafaulu kujiunga na Uru Seminary mwaka 1993. Mwaka 1996 Form Four yetu tukawa wa kwanza Tanzania nzima na mimi nikachaguliwa kujiunga Ilboru Special School!! Was my Std 7 failure fate? Sijui! But I am glad I failed.
Ningefaulu Std 7 nisingeenda Uru Seminary. And who knows safari yangu ingeishia wapi? Nisingekuwa na marafiki nilionao hapa. And may be I would never have been a lawyer. Najua kilichotokea baada ya kufeli ila sijui ambacho kingetokea kama ningefaulu Std 7. Thats life. Do not complain.

Mara zote naangalia maisha yangu kuanzia baada ya Std 7 na kilichotokea. Na kujifunza kwamba ‘failure’ (i call it fate) takes you to where you are. When it happens go with the flow kufika kule unakoenda na unakopaswa kuwepo.
Kwa ujumla maisha ni ndoto. Kila ukiamka unataka kupiga hatua zaidi. Ukipata nyumba unataka nyumba uzunguni. Ukipata gari unataka gari ya 2018. Ni rahisi sana kusahau kuhusu ulichonacho na kuendelea kukumbuka ambacho hauna. Utakosa furaha.
Picha hii inanipa nguvu kubwa kuhusu mambo mawili. 1. Kubadilika mwenyewe. Kuachana na mambo ya ujana na utoto (ugangwe, kusuka nk) na kupevuka kiakili zaidi. 2. Kubadilika kwa lazima kutokana na wakati. Kupata upara, kuzeeka na majukumu yanayokujia. Hayo yote lazima yatokee kwenye maisha yako.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad