Beki kisiki wa timu ya Taifa ya Tanzania na klabu ya Baroka FC ya nchini Afrika Kusini, Abdi Banda ameamua kuvunja ukimya na kuwajibu wale wote wanaosema amejitoa kwenye kikosi cha Taifa Stars.
Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram, Banda amewajibu kuwa yanayosemwa hayana ukweli wowote ila alikosa nafasi kutokana na ubora wa wachezaji waliyopo katika mazoezi na mwalimu anahaki ya kuchagua.
”Maneno yamekuwa ni mengi sana na kila mtu anasema lake ila kikubwa sikupata nafas kutokana na ubora wa wachezaj waliouonyesha mazoezini na mwalimu anahaki ya kuchagua yupi acheze na yupi asicheze,” ameandika Banda kwenye mtandao wake wa Instagram.
Abdi Banda mwenye umri wa miaka 23 ameongeza kuwa ”Kitendo cha kuanza kuandika au kudanganya watanzania nimemshaur mwalimu kuhus wachezaj bado sijawa na uwezo huo maana kuna walimu zaidi ya wanne wana kazi gani pale? Na mwalimu akisema tucheze mabeki 11 tutacheza labda kuna kitu kakiona sasa haya maneno sijui nimejitoa timu ya taifa yanatoka wap au ni kuanza kupandikiza chuki zidi yangu na walimu na watanzania ikiwa najijua sipendezwi kwa baadhi ya watu.”
”Kikubwa tujue tumekosea wap ila hizi chuki hazijengi na usijaribu kuharibu maisha ya mwenzako.
Mm ntacheza taifa stars labda nisiitwe na kucheza timu ya taifa ni heshima kwa sisi tunaocheza hivi vi timu vidogo huku nje🇹🇿.”
Katika maelezo yake aliyoposti kwenye mtandao wake wa Instagram ameambatanisha na kipande cha habari kinachoelezea kuwa amejitoa kwenye timu ya Taifa.