Abdulhalim Humud awaumiza KMC

Abdulhalim Humud awaumiza KMC
Kocha wa klabu ya KMC Etienne Ndayiragije ameweka wazi kuwa anahitaji kuziba pengo la Abdulhalim Humud ambaye ameondoka hivi karibuni klabuni hapo baada ya pande mbili kuvunja mkataba.

Akiongea leo na www.eatv.tv ikiwa ni siku ya kwanza tu ya dirisha dogo la usajili ambalo limeanza leo Novemba 15 - Desemba 15, Ndayiragije amesema kwasasa amebakiwa na kiungo mmoja tu mwenye uwezo wa kucheza namba 6 hivyo lazima apate mwingine.

''Nimewasilisha mapendekezo kwa uongozi kwaajili ya wachezaji ninaowahitaji ambapo kuna nafasi nyingi ikiwemo kiungo namba 6 baada ya Humud kuondoka, pamoja na namba 9 mwenye uwezo wa kushindana'', amesema.

Ndayiragije pia ametaja nafasi nyingine ambazo anahitaji kuzipatia wachezaji ni pamoja na mlinzi wa kushoto na mlinzi wa kati ambao wote anataka watoke hapa Tanzania.

Aidha kocha huyo amesema mabadiliko ya ratiba ya ligi yanawasaidia kupata mapumziko na kujipanga vizuri kwaajili ya mechi zinazokuja hivyo yeye hana tatizo na ratiba ya ligi kupanguliwa hususani pale kunapokuwa na mechi za kimataifa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad