Abiria nchini kuanza kutozwa faini

Abiria nchini kuanza kutozwa faini
Imeelezwa kuwa abiria anaweza kuwa muhanga wa uvunjifu wa sheria ya usalama barabarani  hadi kulipishwa faini, endapo atashindwa kuzingatia sheria hizo ikiwemo kutofunga mkanda au kushuhudia uvunjifu wa sheria na kutotoa taarifa.


Akizungumza kwenye East Africa BreakFast ya East Africa Radio, Mkuu wa kitengo cha Elimu na Mafunzo Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Abel Swai amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya Mamlaka ya uthibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) sio dereva tu, hata abiria anatakiwa kuchukuliwa hatua akishindwa kukemea au kutoa taarifa sehemu husika.

Swai amesema kuwa, "Abiria anakuwa mhanga wa faini kutokana na uvunjifu wa sheria za usalama barabarani endapo akiwa sehemu ya uvunjifu wa sheria hiyo kwa mujibu wa sheria ya SUMATRA, na ndio maana tumetoa namba endapo ukiona kuna viashiria vya uvunjifu wa sheria ikiwemo mwendokasi toa taarifa".

Ameongeza kuwa, "Kuna baadhi ya abiria wanakuwa chanzo cha makosa ya barabarani kwakutofunga mikanda na kuchochea mwendokasi.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani, hadi kufikia Novemba 30, mwaka jana Watanzania 2,994  walifariki kwa ajali zilizohusisha mabasi, malori, magari madogo, bajaji na bodaboda.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad