Ajari Ziwa Victoria: Rais Museveni ataka nahodha wa boti iliyozama afunguliwe kesi ya mauaji
0
November 26, 2018
Watu 31 wameripotiwa kufariki, huku wengine 29 wakinusurika kwenye ajali mbaya ya kuzama kwa boti iliyotokea jana jioni ziwa Victoria kwa upande Uganda.
Imeelezwa kuwa Boti hiyo yenye uwezo wa kubeba watu 50, ilibeba watu 150 jambo lililopelekea kuzama muda mfupi baada ya kuanza safari mjini Mpatta wilayani Mukono.
Shughuli za uokoaji zinaendela mpaka sasa ambapo Kamishna Msaidizi wa polisi nchini humo, anayesimamia oparesheni hiyo, Asuman Mugenyi amesema kuna uwezekano mdogo wa kupata miili ya watu waliohai.
Kufuatia ajali hiyo, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametuma salama za rambi rambi na kumtaka nahodha wa boti hiyo wachukuliwe hatua za kisheria. of all those departed rest in peace.
Tags