Albamu ya Lil Wayne Yafanya Makubwa Auza Kopi Zaidi ya Milioni 1

Albamu ya Lil Wayne Yafanya Makubwa Auza Kopi Zaidi ya Milioni 1
Takribani miezi miwili tu tangu Albamu mpya ya Rapa Dwayne Michael Carter Jr maarufu kwa jina la ‘Lil Wayne‘ inayoitwa ‘Carter V’ iachiwe, imefanikiwa kufikia mauzo ya Platinum (kuuza kopi zaidi ya million 1).



Kwa upande wa Record Industry Association Of America (RIAA) bado hawajaitunukia albamu hiyo lakini Lil Wayne amesherehekea mauzo hayo kupitia akaunti yake ya wa Instagram, ameweka picha ikiambatana na maelezo yaliyosomeka, “Thank u.”


Albamu hiyo iliyotengenezwa na producer Swizz Beatz, iliingia sokoni Septemba 27 na na kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwenye chart kubwa za Billboard 200 baada ya kufanya mauzo makubwa ndani ya wiki ya kwanza ambayo yalikuwa ni zaidi ya kopi 480,000 huku ikisikilizwa mara million 433

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad