DIAMOND alimwalika Kiba kwenye shoo ya Wasafi. Lilikuwa jambo jema. Mwingine angeona dogo wa Tandale anapandisha mabega, anajiona anaweza kumlipa Kiba ili apige kazi kwenye Wasafi Festival.
Chuki ni upofu, upendo huona kila kitu. Kiba angetanguliza chuki, asingeona uzuri wa Wasafi Festival wala heshima ya kumwalika ashiriki naye jukwaa moja. Alipoweka upendo mbele, alijua thamani ya mwaliko, akajibu kwa nidhamu.
Kiba alipokea mwaliko na kuomba radhi kwamba ratiba yake ya kutangaza kinywaji chake cha MoFaya inambana, hivyo asingeweza kupanda jukwaani Wasafi Festival, lakini kwa malengo ya kukuza muziki, akaomba kudhamini shoo hiyo ya Wasafi.
Narudia; chuki ni upofu, upendo huona kila kitu! Diamond angepumbazwa na chuki, asingeona nia njema ya Kiba kuipiga tafu ya kifedha Wasafi Festival, angeona Kiba alitaka kujifanya baabkubwa kwamba ana fedha mpaka anamdhamini.
Upendo huona kila kitu, kwamba Diamond akaona tobo la mafanikio ya Wasafi Festival kupitia jeki ya MoFaya. Akakubali, akamwagiza meneja wake Sallam afanye mazungumzo na meneja wa Kiba, bi'dada Seven. Mpaka hapo wote wawili wakawa wameshinda sana. Na walikwepa mitego vizuri kabisa. Siwapingi wenye kusema uamuzi wa Diamond na Kiba una watu nyuma yao.
Wote wameonesha uungwana, ila hili usiache kuliona; ilikuwa rahisi Kiba kukataa kufanya shoo ya Wasafi kwa sababu angejibu kama alivyojibu kuwa ratiba haimruhusu na angeeleweka. Diamond ni msanii, anajua ratiba za kazi, hata yeye ameshakataa shoo nyingi kwa sababu ya kubanwa na kalenda.
Hata hivyo, Diamond asingeeleweka hata kidogo kama angekataa udhamini wa Kiba kupitia kinywaji cha MoFaya. Unakataaje udhamini? Kuna kushindwa kuafikiana kwenye vigezo na masharti ya udhamini, lakini siyo kukataa kwamba hutaki kudhaminiwa na Kiba. Yaani Diamond angeuchomolea udhamini wa MoFaya, angeonekana wa hovyooo!
Baada ya wote kushinda na kuvuka mitego sawia, naomba nitoe homework; je, MoFaya ikipita kama mdhamini mkuu wa Wasafi Festival, kisha masharti yakawa tamasha liitwe MoFaya Wasafi Festival itakubalika? Kwa vile MoFaya Afrika Mashariki inabeba jina la Kiba, vipi likiitwa Ali Kiba MoFaya Wasafi
By @luqmanmaloto