Aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini (TSNP), Abdul Nondo amesema licha ya mahakama kutoa hukumu ya kumuachilia huru amedai hatorudi nyuma na harakati zake kwa kile alichokidai anapigania haki.
Nondo ametoa kauli hiyo akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Iringa mara baada ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya mkoa wa Iringa, Liada Chamshana kusema upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha madai yao.
Nondo amesema “siwezi kurudi nyuma hata kidogo, kuna kipindi ilikua ni mimi nikubali kurudi shule na niache mambo yale, lakini niliamini Mungu yupo, na siwezi kurudi nyuma hata kidogo na nitaendelea kufanya zaidi na zaidi. Nimeongezeka nguvu kubwa sana.”
Kwa upande wake mratibu wa mtandao wa utetezi wa haki za binadamu, Onesmo Ngulumo anasema hatua zilizochukuliwa na uongozi wa chuo kikuu cha dare s salam kumsimamisha masomo nondo zimeenda kinyume na sheria na kwasasa wanafanya utaratibu wa kumrejesha masomoni
.
Mara baada ya hukumu hiyo Abdul Nondo alitokwa na machozi wakati akitoka nje ya Mahakama hiyo baada ya kutomkuta na hatia dhidi ya makosa aliyokuwa akishtakiwa.
Nondo alikamatwa marchi 7 mwaka huu akiwa ubungo jijini dare s salaam kwa kile kinachoelezwa kuwa alifanya makosa ya kuchapisha taarifa za uongo kwa njia ya kompyuta pamoja na kutoa maelezo ya uongo kwa afisa wa polisi kinyume cha makosa ya mtandao namba 16 ya mwaka 2016 ambapo
Alichokisema Abdul Nondo Baada ya Kushinda Kesi na Kuachiwa Huru
0
November 05, 2018
Tags