Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wakili Revocatus Kuuli, amesema kufungiwa maisha kujihusisha na masuala ya mpira kwake haijamuathiri chochote.
Kuuli ambaye amefungiwa jana kutokana na sakata la kusimamisha uchaguzi pamoja na maneno ya dhihaka kwa shirikisho hilo, ameeleza kuwa maamuzi hayo alikuwa anayetegema.
Wakili huyo msomi ameonesha kutokuwa na hofu yoyote akieleza kuwa hakuwahi kuajiriwa na TFF na hakuwa anakitegemea chombo hicho kuendesha maisha yake.
Licha ya kufungiwa, Kuuli ameeleza pia hana muda wa kufikiria kwenda kukata rufaa kwani haitokuwa na maana yoyote kwake kufanya hivyo.
"Sina muda wa kufikiria kwenda kukata rufaa kwa maana haitonisaidia lolote lile, mimi sikuajiriwa na TFF na sikuomba kazi hapo" alisema.