VIDEO Vixen wa Bongo, Nascat Abubakary ‘Amber Rutty’ na ‘bwana’ke’, Said Mtopari, wamerudisha katika Gereza la Segerea baada ya kukosa mdhamini katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, Novemba 26, 2018.
Kesi hiyo iliyokuwa ikiendelea leo Jumatatu, Mahakamani hapo, ilikuja kwa ajili ya kutajwa ambapo watuhumiwa (Amber Rutty na mpenzi wake) walitakiwa kuwa na wadhamini wawili kila mmoja na kusaini bondi ya Tsh. Milioni 15 kila mmoja, lakini alijitokeza mdhamini mmoja pekee huku mmoja akikosekana.
Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Agustino Lwizile amesema kuwa dhamana ya mtuhumiwa ipo wazi na kama kufikia saa 9 jioni mdhamini wa pili atajitokeza, basi atapatiwa dhamana na kuahirisha hadi Desemba 10, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.
Amber Rutty na mpenzi wake wanakabiliwa na makosa ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile,
kuchapisha video / picha za ngono na kusababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp.
Amber Rutty na Mpenzi Wake Wakwama Mahakamani Wakosa Dhamana Warudishwa Segerea
0
November 26, 2018
Tags