Askofu Evarist Chengula Afariki Dunia

Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Mbeya, Evarist Chengula amefariki dunia katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika Hosptali ya Taifa Muhimbili.
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Dk Charles Kitima amesema Askofu Chengula alifariki leo Jumatano Novemba 21, 2018 akiwa anapatiwa matibabu ya moyo.
“Ni kweli askofu wa jimbo la Mbeya baba Chengula amefariki leo saa tatu asubuhi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili,’’ amesema.
Amesema kuwa askofu Chengula alikuwa anasumbuliwa na tatizo la moyo na aliwasili Muhimbili jana Jumanne (Novemba 20, 2018) akitokea mkoani Mbeya.

‘Si kuwa alikuwa mgonjwa sana, alikuwa na tatizo la moyo lakini juzi alikuwa ametoka kazini huko vijijini likaanza kumzidia, sasa jana (Jumanne) akaamua aje hospitalini,’ amesema Dk Kitima

Mwezi Machi mwaka huu, Askofu Chengula aliwataka wakristo kote nchini kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2019 wa Serikali za Mitaa akiwataka wananchi kumchagua mtu asiyewafanya waishi kwa kuogopaogopa.

Alitoa kauli hiyo Machi 30, 2018 alipokuwa akiongoza ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika kitaifa katika kanisa Katoliki la Bikira Maria wa Fatma lililopo Mwanjelwa mjini Mbeya.

Pia katika ibada hiyo, alitolea ufafanuzi ujumbe uliotolewa na maaskofu wakatoliki akisema ujumbe ulikuwa haumlengi mtu fulani bali uliwalenga wanafiki wanaodai ni Wakristo lakini hawana imani ya Kikristo ili waweze kubadilika na kuwa watu wema.

Mwananchi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad