Azam FC Yatoa Sababu za Kumsajili Chirwa

Azam FC yatoa sababu za kumsajili Chirwa
Vinara wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam FC wamefikia makubaliano ya kumsajili nyota wa zamani wa Yanga Mzambia, Obrey Chirwa.


Chirwa amejiunga na Azam kama mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake na klabu ya Nogoom El Mostkabl FC ya Misri baada ya klabu hiyo kushindwa kumlipa stahiki zake za kimkataba.

Uongozi wa Azam FC, leo umetangaza kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji, Obrey Cholla Chirwa, kwa mkataba wa mwaka mmoja ambapo leo hii pia ametambulishwa mbele ya waandishi wa habari.

Mwenyekiti wa Azam FC Abdulkarim Amin ameweka wazi kuwa sababu ya kumsajili Chirwa ni mahitaji ya mwalimu Hans Van Pluijm.

''Usajili huu ni sehemu ya mapendekezo ya Benchi la Ufundi la klabu chini ya Kocha mkuu Hans Van Der Pluijm, katika kuboresha eneo la ushambuliaji la timu yetu ili kufanikisha harakati za kusaka mataji'', amesema.

Awali iliripotiwa Chirwa aliomba kujiunga na Yanga SC ila kocha mkuu wa klabu hiyo Mwinyi Zahera alimkataa kwa kusema hana uvumilivu timu ikiwa kwenye matatizo. Chirwa ataanza kutumika rasmi baada ya dirisha dogo kufunguliwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad