Baada ya Kufungwa Wimbo was Nyegezi Mzazi Mwenzake Rayvanny Atoa ya moyoni kwa Basata

Baada ya Kufungwa Wimbo was Nyegezi Mzazi Mwenzake Rayvanny Atoa ya moyoni kwa Basata
SIKU chache baada ya Basata kufungia wimbo wao wa Mwanza, muuza nyago kwenye video za Bongo, Fahyma ‘Mama Jaydan’ amemkingia kifua mzazi mwenziye ambaye ni msanii wa muziki kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Raymond Mwakyusa kuwa wamemnyima haki ya kuonesha kipaji chake.



Akizungumza na Ijumaa , Fahyma aliyewahi kutokelezea kwenye video kadhaa ikiwemo Kwetu ya Rayvanny alisema kuwa, wimbo wa mzazi mwenziye uliofungiwa ni kwa ajili ya kuburudusha vijana na sio watoto kwa hiyo ziwekwe sheria ambazo zitawapa wasanii uhuru wa kubuni vitu vizuri kwa kuwa sio wote wameuelewa wimbo huo kutokana na ubunifu uliotumika.



“Nimejisikia vibaya sana kwa sababu ni kazi ya mume wangu halafu ni kazi ambayo naipenda sana, lakini pia wamepoteza pesa nyingi na muda kurekodi halafu wanafungia wimbo kirahisi tu, wanaposema wimbo hauna maadili huwezi jua kila mtu anaposikiliza anakuwa ana mtazamo wake.



“Mimi sioni tatizo kwenye huo wimbo kwa sababu umetungwa kwa ubunifu wa hali ya juu mbona nchi za wenzetu hawana haya mambo jamani tena kama Nigeria wanaandika kabisa kuwa muvi hii ni kwa ajili ya watu walio juu ya miaka kumi na nane?” aliongea Fahyma.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad